TAHADHARI YA MATAPELI WA TSSF WANAOJIFANYA KUTOA MIKOPO
TSSF ni kampuni inayojitangaza kuwa imesajiliwa Tanzania na inajishugulisha na shuguli za utoaji mikopo nchini Tanzania kwa ngazi za degree na diploma kwa wale waliokosa mkopo kutoka bodi inayotambulika ya mikopo ya chuo.
Nawaasa vijana wa ki Tanzania, wadogo zangu, ndugu zangu kuwa kampuni hii sio kampuni halalai, ni kampuni ya matapeli na ni fake, napenda kuanza kuwakumbushia vijana wenzangu kuwa.
Kampuni nyingi za kitapeli hapa Tanzania wanatumia hosting (kampuni ya kurusha website yao) ya bure ambayo ni weebly.com, kila uonapo website inaishia na hilo neno tafadhali ndugu yangu mtanzania kwepa, kimbia usipemde kusoma na kushiriki kila jambo watakalosema humo ndani.
Kampuni za kiserikal au zile halali zisizo za kiserikali hutumia domain(jina la website) ambalo ni worldwide kama .org, .com, .info na kadhalika na kama ni serikal watatumia .co.tz au .go.tz yaani itamalizia.tz.
Kwa hiyo nawapasa vijana wenzangu, wadogo zangu msidanganyike na mkaliwa pesa zenu bure ambazo zingekusaidia kwa jambo jingine.
Please naombeni msambaze link hii ili vijana wengi wapate kukombolewa kutoka katika utapeli huu wa hawa jamaa...
Hapa chini naweka website walio tangazia kuwa wanatoa mkopo.
Https://tssf-org-tz.weebly.com.
Hii ndio webiste walio tangaza wao.
Sambaza zaidi vijana wakombolewe.
By wasamaria wema...

Hakuna maoni