Chupa ya mvinyo ghali zaidi duniani yaibwa Denmark
Polisi nchini Denmark wanachunguza
kisa cha wizi wa chupa ya mvinyo inayodaiwa kwa ghali zaidi duniani ya
thamani ya dola milioni 1.3.
Chupa hiyo iliyotengenezwa kutoka kwa
dhahabu na fedha na kifuniko cha almasi ilikopeshwa baa moja huko
Copenhagen ambayo ilikuwa imekusanya chupa za mvinyo kwa maonyesho.Mmiliki wa baa hiyo Brian Ingberg alisema chupa ilikuwa imetumiwa kwenye kipindi kinachofahamika kama House of Cards.
- Biashara ya pombe yashuka kote Duniani
- Kwa Picha: Harusi 'ghali zaidi' India
- Coca-Cola ilivyopata jina lake
Polisi wanasema kuwa haijuikani ikiwa mwzi huyo ambaye alivamia siku ya Jumanne alivunja au alikuwa na ufunguo.
Bw. Ingberg ambaye ni mmliki wa bar aliiambia runinga ya TV2 kuwa alikuwa ameikopa chupa hiyo kutoka kwa kampuni moja huyo Latvia.
Hakuna maoni