fb,twita,insta

tangazo

MIONGONI BI'DAA ZA HARUSI






 



                                 MIONGONI MWA BID'AA ZA HARUSI.
  • wazazi wa mke au babu zake kumlazimisha mume atoe kifungua mlango ili apewe ruhusa ya kumuona mkewe.
  • mashemeji wa kike wa upande wa mke kumfanyia maskhara mume wa ndugu yao hata kukumbatiana na kumbusu.

Haya ni maasi makubwa.
  • kuna baadhi ya mila katika miji mingine, humfichia viatu mume mpaka unafika muda wa kuondoka na mkewe bila kumrejeshea viatu vyake.
  • kuingia baadhi ya wanadai kuwa ni mashekhe ndani ya chumba cha mke watu, kwa madai ya kumuombea dua.
  • baadhi ya mabibi wa wake, huingia chumbani mwa maharusi wawili siku ya mwanzo wa harusi,  na hulala humohumo usiku huo, kwa lengo la kuwafundisha.
  • na kuna baadhi ya mabibi wa wake,  imeshatokea kuzini na waume wa wajukuu zao, kwa sababu ya kuingiwa ibilisi baada ya kushuhudia tendo la ndoa kati ya wawili hao usiku wa harusi.
  • kuna baadhi ya mila za watu wanafanya kuweka shuka nyeupe usiku wa mwanzo wa harusi, na kuwataka maharusi wawili hao wakitoa haja zao (manii) wakati wa maingiliano,  basi wamalizie haja zao hizo katika shuka nyeupe hiyo.

  • Kisha siku ya pili asubuhi inatangazishwa shuka hiyo na kutangazwa mbele za watu wote kuwa ndoa imefaulu.
  • na wengine humlazimisha mwanaume kuvaa kanga za mkewe muda wa siku saba kamili, na mume hawamruhusu kutoka nje hata kidogo hata ikiwa ni kwa ajili ya sala.
  • wengine pia huwa wanajipaka unga mweupe uso mzima ili kujikinga na shari za siku hiyo ya mwanzo ya ndoa.
  • wengine ni maimaamu wa misikiti,  huwa wanalazimisha wakati wa kufungisha ndoa lazima bwana harusi aelekee kibla.

Hakuna maoni